Makuadi wa Soko huria (Chachage S. L. Chachage)

Tanzanie
  • kiswahili

Chachage Seithy L. Chachage, Makuadi wa Soko huria, Dar es Salaam : ED Limited, 2002.

Texte en version originale

Version originale

Original version


Tayari Mzee Baharia alikuwa akiifungua kamba na kuivutia chomboni. Aliiwasha injini ya boti, ambayo iliitikia mara moja, kisha akaketi vizuri kule nyuma ya chombo na kuanza kukiongoza. Sisi wote tukawa tunapunga mikono kuwaaga wale waliokuwa pale ukingoni mwa mto.

Lo ! Ilikuwa ni bahati ilioje hii kusafiri na mmojawapo na wenyeji wetu. Safari ilianza, mwanzoni wote tukiwa kimya kabisa, hali iliyoonyesha wazi tulikuwa waoga wa maji. Sauti pekee tulizozitoa ni zile za kujipiga makofi mwilini kufukuza mbu ambao walikuwa wengi kwelikweli. Giza nalo lilitutisha kidogo, lakini Mzee Abdurahman alielekea kuyaelewa fika mazingira ya sehemu alimokuwa akitupitisha. Kulipoanza kuwa mwanga kidogo, tuliweza kuyaona yale yaliyokuzunguka : mikoko mitupu, na matawi ya mto yaliyoingia au kutokezea hapa na pale, makubwa na madogo, marefu na mafupi. Uso wa mbingu ulianza kukunjuka kuikaribisha nuru ya jua liliyokuwa ndiyo kwanza linachomoza. Sasa kulikikia sauti za bata mwitu, kitwitwi na ndege wengine, wakia kama wanaimba. Tuliweza pia kusikia sauti za mungurumo, mguno na kelele za wanyama. Hivi vyote viliihinikiza hii mandhari tuliyokuwa tukiipita.

Makuadi wa Soko huria, p. 219

Texte en français

Traduction française


Le vieux Baharia détacha la corde et la tira dans le vaisseau. Il mit le moteur du bateau en marche, qui réagit immédiatement, puis s’assit à l’arrière pour manoeuvrer le gouvernail. Nous fîmes un signe d’au revoir à ceux qui se trouvaient au bord de la rivière.

Quel privilège de voyager avec l’un de nos hôtes ! Le voyage commença dans un silence qui s’expliquait par notre peur de l’eau. On n’entendait que les claques pour repousser les nombreux moustiques. L’obscurité nous faisait aussi un peu peur, mais Abdurahman semblait savoir par où il voulait nous faire passer. Quand il commença à faire jour, nous pûmes voir ce qui était autour de nous : de la mangrove et des bras de rivière qui entraient ou sortaient ici et là, larges ou étroits, longs ou courts. La surface du ciel commença à briller pour accueillir la lumière du soleil levant. Maintenant, on entendait les voix de canards sauvages, de lézards et d’autres oiseaux, comme s’ils chantaient. Nous pouvions également entendre le murmure du tonnerre, les grognements et les sons des animaux. Tout venait à l’appui du paysage que nous traversions.

Texte en anglais

English translation


Old Baharia untied the rope and pulled it into the ship. He started the boat’s engine, which responded immediately, then sat in the stern to operate the rudder. We waved goodbye to those by the river. What a privilege to travel with one of our hosts! The journey began in silence which could be explained by our fear of water. We only heard the slaps to repel the numerous mosquitoes. The darkness also scared us a little, but Abdurahman seemed to know where he wanted us to go. When it began to get light, we could see what was around us: mangroves and river arms that came in and out here and there, wide or narrow, long or short. The surface of the sky began to glow to welcome the light of the rising sun. Now the voices of wild ducks, lizards and other birds could be heard, as if they were singing. We could also hear the murmur of thunder, grunts and animal sounds. Everything supported the landscape we were crossing.

Texte en version originale

Version originale

Original version


Hatukulala muda mrefu. Mzee Miraji aliniamsha mimi, Mjuba na Makoba mnamo saa kumi na moja asubuhi, mimi kwanza, kwa kuwa nilikuwa nimelala nyumbani kwake kisha Makoba na Mjuba waliokuwa nimelala nyumba ya jirani. Alitutaka tuteremke naye hadi baharini atakuonyeshe meli za wageni zilizokuwa kwenye pwani, kwa kuwa yeye na jirani yake walikuwa wanakwenda baharini kuangalia nyavu na nyando walizokuwa wamezitega.

            Tuliondoka kwa jahazi, tukafika pwani ya Bahari ya Hindi wakati jua linachomoza. Mzee Miraji na jirani yake waliteremsha tanga, na kuzipitia nyavu na mitego ya wando. Pale pwani kulitapakaa mitego ya aina hiyo na mingine ya matete iliyotapakaa na kufanya wigo wa aina yake. Kadhalika, tayari kulishakuwa na wavuvi wengine wengi na mbali kule baharini kulikuwa na meli kubwa za uvuvi, karibu kumi hivi.

            Mzee Miraji na mwenzake walikuwa wamepata samaki kidogo sana ingawa walikuwa na mitego ya wando ishirini na nyavu sita. Kila walipowavua hao samaki, waliwa rudisha baharini wale ambao walikuwa hawawahitaji, au walikuwa bado wachanga.`

            « Ingawa mavuno ni madogo, lakini taabu kubwa itakuwa ni kupata soko, tutaishia kuwakausha na hatimaye kuwapeleka hapo baadaye Dar es Salaam na bara. Miaka michache iliyopita, tulikuwa tukipata barafu, na tukaweza kuuza hata samaki wabichi, kabla vurugu za yule Mgiriki aliyekuwa akitukopa na kuingia huyu Mzungu mwingine kuchukua kiwanda, » Mzee Miraji alifafanua.

« Sasa hivi samaki wamepungua sana kwa sababu ya madubwana yale kule, » Mzee Miraji aliendelea kueleza, huku akiwa kanyoosha kidole yanakokota kila kitu, na yanafika hata huku ufukoni hadi kwenye matawi ya mito huku Delta, kisha huwatupa samaki waliokufa baharini. « Miezi mitatu iliyopita alikuja afisa uvuvi hapa, akadai kwamba hawa samaki wote wanaoelea baharini mara kwa mara wakiwa wamekufa ni kwa sababu ya madawa ambayo tunayatumia sisi katika kilimo chetu cha mpunga na mazao wengine, akatuonya kwamba kama hatutaacha kutumia madawa basi serikali itatuzuia kulima. »

Chachage Seithy L. Chachage, Makuadi wa Soko huria, Dar es Salaam : ED Limited, 2002, p. 252-253.

Texte en français

Traduction française


Nous n’avons pas dormi longtemps. Miraji nous a réveillés, Mjuba, Makoba et moi à 5 heures du matin ; moi d’abord, car je dormais chez lui, puis Makoba et Mjuba, qui dormaient dans une maison voisine. Il voulait nous emmener jusqu’à la mer pour nous montrer les navires étrangers sur la côte, car lui et son voisin partaient en mer pour relever les filets et les filets qu’ils avaient installés.

               Nous partîmes en bateau et arrivâmes à la côte de l’océan Indien au lever du soleil. Miraji et son voisin ont abaissé la voile, passant à travers les filets et les nasses. La côte était recouverte de nasses de différents types. Il y avait déjà beaucoup d’autres pêcheurs et plus au large il y avait de gros bateaux de pêche, environ une dizaine.

               Miraji et son compagnon n’avaient attrapé que de tout petits poissons dans leurs vingt nasses et six filets. Ils devaient en plus rejeter à la mer ceux qui n’étaient pas comestibles et ceux qui étaient encore jeunes.

               « Bien que le rendement soit faible, le plus gros problème est de trouver un marché. Nous finirons par les faire sécher pour les transporter vers Dar es Salaam et le continent. Il y a quelques années, nous recevions de la glace et il était possible de vendre le poisson frais, mais le Grec qui nous prêtait a fait faillite et l’usine a été reprise par ce Mzungu », nous expliqua Miraji.

               « Maintenant, le poisson manque à cause de ces navires là-bas, » continua Miraji, expliquant en pointant son doigt. Nous atteignîmes la plage à l’entrée d’un bras du delta, et il jeta les poissons morts dans la mer. « Il y a trois mois, un agent des pêches est venu ici, affirmant que tous ces poissons qui flottent dans la mer sont morts à cause des produits chimiques que nous utilisons dans nos rizières et nos champs, et nous a avertis que si nous n’arrêtions pas d’utiliser des engrais, le gouvernement interdirait l’agriculture. »

Texte en anglais

English translation


We didn’t sleep long. Miraji woke up Mjuba, Makoba and me at 5 a.m.; me first, because I was sleeping at his house, then Makoba and Mjuba, who were sleeping in a neighboring house. He wanted to take us to the sea to show us the foreign ships on the coast, because he and his neighbor were going out to sea to collect the nets and nets they had set.

               We set off by boat and arrived at the Indian Ocean coast at sunrise. Miraji and his neighbor lowered the sail, passing through the nets and traps. The coast was covered with traps of different types. There were already many other fishermen and further offshore there were large fishing boats, around ten.

               Miraji and his companion had only caught very small fish in their twenty traps and six nets. They also had to throw back into the sea those who were not edible and those who were still young.

               “Although the yield is low, the biggest problem is finding a market. We will eventually dry them for transport to Dar es Salaam and the mainland. A few years ago, we received ice cream and it was possible to sell the fresh fish, but the Greek who lent us went bankrupt and the factory was taken over by this Mzungu,” Miraji explained to us.

               “Now the fish is missing because of those ships over there,” Miraji continued, explaining while pointing his finger. We reached the beach at the entrance to an arm of the delta, and he threw the dead fish into the sea. « Three months ago, a fisheries officer came here, saying that all these fish floating in the sea died from the chemicals we use in our rice fields and fields, and warned us that if we did not stop using fertilizers, the government would ban agriculture. »